Sisi ni mtandao wa watu walioathiriwa na Kifua Kikuu (TB) nchini Tanzania ambao tumejitolea kupambana na TB kwa njia ya uhamasishaji, kuratibu, kutetea, na kuongeza uelewa wa namna ambavyo TB inaathiri maisha yetu kwa namna moja ama nyingine.

Mafunzo na Kushirikishana Uzoefu

Waathirika kushiriki katika utekelezaji wa Afua za ushawishi na utetezi, kutoa elimu ya TB katika jamii, kusimamia na kufanya tathmini ya mafanikio na changamoto za Kifua Kikuu katika jamii.

Kujenga Uwezo

Tunapaza sauti moja ya jamii zilizoathiriwa na Kifua Kikuu kutoka maeneo na mazingira tofauti katika wilaya na mikoa yote ya Tanzania ili jamii ifurahie kwa kupata haki na uhuru katika huduma za afya.

Ushirikishwaji wa jamii

Kuongeza ufanisi wa TTCN kama jukwaa la jamii zilizoathiriwa na Kifua Kikuu kwa kukusanya na kutoa taarifa sahihi za TB, kuwa na wanachama hai na wanaoshiriki katika ngazi zote kwenye jamii.

Washirika na Wadau wetu

NTLO
ACT
global TB Causus
EANNEASO
MKUTA
Stop TB Partnership