Muundo

Mtandao wa Kijamii wa Mapambano dhidi ya Kifua Kikuu Tanzania (TTCN) unaongozwa na Bodi ya Wakurugenzi ambao wanawajibika katika kuandika kanuni na taratibu zinazoongoza maendeleo ya Mipango Mkakati na maendeleo ya Miongozo na Sera za Shirika. Pia Bodi hii inachagua wakaguzi na wanachama wapya na wafanyakazi wa Sekretarieti, wakiwemo: wakurugenzi watendaji ambao ni wajumbe wa sekretarieti. Sekretarieti: ni chombo kamili kinachotazamwa katika kutekeleza Mipango Mkakati ya TTCN. Ofisi za Sekretarieti TTCN hivi sasa zipo nchini ya usimamizi wa EANNASO.