Tunalenga kuhakikisha kuna mazingira wezeshi na muundo sanifu na bunifu wa asasi za kiraia na ushiriki wa uratibu vikundi jamii pamoja na sera na wafanya maamuzi ili kukuza upatikanaji wa huduma ubora na unafuu kwa watu wenye Kifua Kikuu. Tunatetea ujumuishwaji wa asasi za kiraia na vikundi vya kijamii ndani ya michakato ya kuandaa sera za kitaifa ili kuhakikisha kwamba sera na sheria zilizoundwa zinaendana na watu na sio za kukandamiza kundi lolote katika jamii. Tunaunga mkono juhudi za serikali na wanaharakati wa TB na afya katika kutekeleza ahadi na mikakati ya kutokomeza Kifua Kikuu na utekelezaji wa Mpango wa Afya kwa Wote (UHC) pamoja na uwekezaji wa kifedha ulio endelevu.