Tunatoa mafunzo, taarifa na kupeana uzoefu kwa ajili ya utekelezaji wa pamoja. Tunaboresha majukumu yetu kama watoa maarifa, mkusanyiko wa washirika na wadau kushiriki katika kutoa uzoefu na kuwezesha mafunzo na kujenga uzoefu miongoni mwa washirika na wadau kwa ujumla. Tunakusudia kusaidia kutengeneza na kukuza ujumbe wenye nguvu unaoweza kutekelezwa ili kushughulikia vizuizi na mapungufu ya ufadhili kwa AZAKi; mazingira mazuri ya kisheria na sera, upatikanaji wa huduma za Kifua Kikuu pamoja na taarifa zinazopelekea kufanya utetezi wenye misingi ya ushahidi na maamuzi kwa ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa. Mchango wetu na shughuli kubwa zinalenga zaidi katika (a) kukuza ushiriki na mafunzo kwa AZAki; (b) kuweka kumbukumbu na kutoa taarifa za TB, taarifa zilizopatikana na ushuhuda wa mafanikio na (c) kuongeza mawasiliano na teknolojia ili kuwezesha mafunzo yenye tija. Tembelea ukurasa wetu wa Nyaraka zetu ili kujifunza zaidi kuhusu Kifua Kikuu na jitihada zilizofanyika hapa Tanzania na ulimwenguni kote kutokomeza janga la Kifua Kikuu.