Utekelezaji wa programu yetu unaenda sambamba na jukumu la kuratibu AZAKi ili ziweze kupambana pamoja na kwa ufanisi juu ya janga la Kifua Kikuu ili kuchangia kufikia malengo na maendeleo ya kitaifa na kimataifa. TTCN inafanya kazi hii kwa (a) kuimarisha na kuongeza kasi ya utekelezaji wa mambo yaliyo ndani ya uwezo wetu ili kupata matokeo zaidi kupitia rasilimali zilizopo (b) kuhamasisha na kushirikisha idadi kubwa ya mashirika na washirika waliopo nchini na kimataifa (c) kuimarisha ubunifu, ushirikiano na muungano kati ya wanachama na washirika katika ngazi mbalimbali. Jiunge Nasi kufahamu watu na mashirika yanayofanya kazi ya kutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu nchini Tanzania.