Ushiriki wa Jamii, Asasi za Kiraia/Kijamii

Tunajitahidi kuimarisha ushiriki na ubunifu wa asasi za kiraia na jamii zilizoathiriwa na Kifua Kikuu kwa kutoa suluhisho la pamoja litakalosaidia kutokomeza Kifua Kikuu. Ushiriki na kuhusishwa kwa jamii na AZAKi katika kuandaa na kutunga sera kwa mtazamo wa kuwa na mazingira ya programu kuelekea upatikanaji wa huduma bora za kuzuia TB, kutoa matibabu, uangalizi na kusaidia jamii zilizoathiriwa na Kifua Kikuu. Tunaamini katika mfumo shirikishi, kufanya kazi pamoja na NTLP, TAMISEMI na majukwaa mengine ya kimataifa, kama vile Muungano wa Afrika juu ya Kifua Kikuu (Africa Coalition on TB), Shirika la Afya Duniani (WHO), watu wenye Kifua Kikuu (TB People) na Mfuko wa Kimataifa wa usalama wa asasi za kiraia na ushiriki wa Kitaifa na Kikanda kuhusiana na ajenda za afya, kama vile Mpango wa Afya kwa Wote, jinsia, na haki za binadamu. Kwa taarifa zaidi, tembelea ukurasa wetu wa matukio kujua kuhusu fursa za kushiriki katika matukio ya jamii ya wapambanaji dhidi ya Kifua Kikuu. Kutoka Wavuti, mpaka kitaifa na mikutano ya kimataifa, mikutano ya vikundi kazi na mijadala, kuna kitu kwa ajili ya kila mtu.

Sera na Utetezi

Tunalenga kuhakikisha kuna mazingira wezeshi na muundo sanifu na bunifu wa asasi za kiraia na ushiriki wa uratibu vikundi jamii pamoja na sera na wafanya maamuzi ili kukuza upatikanaji wa huduma ubora na unafuu kwa watu wenye Kifua Kikuu. Tunatetea ujumuishwaji wa asasi za kiraia na vikundi vya kijamii ndani ya michakato ya kuandaa sera za kitaifa ili kuhakikisha kwamba sera na sheria zilizoundwa zinaendana na watu na sio za kukandamiza kundi lolote katika jamii. Tunaunga mkono juhudi za serikali na wanaharakati wa TB na afya katika kutekeleza ahadi na mikakati ya kutokomeza Kifua Kikuu na utekelezaji wa Mpango wa Afya kwa Wote (UHC) pamoja na uwekezaji wa kifedha ulio endelevu.

Mafunzo na Kushirikishana Uzoefu

Tunatoa mafunzo, taarifa na kupeana uzoefu kwa ajili ya utekelezaji wa pamoja. Tunaboresha majukumu yetu kama watoa maarifa, mkusanyiko wa washirika na wadau kushiriki katika kutoa uzoefu na kuwezesha mafunzo na kujenga uzoefu miongoni mwa washirika na wadau kwa ujumla. Tunakusudia kusaidia kutengeneza na kukuza ujumbe wenye nguvu unaoweza kutekelezwa ili kushughulikia vizuizi na mapungufu ya ufadhili kwa AZAKi; mazingira mazuri ya kisheria na sera, upatikanaji wa huduma za Kifua Kikuu pamoja na taarifa zinazopelekea kufanya utetezi wenye misingi ya ushahidi na maamuzi kwa ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa. Mchango wetu na shughuli kubwa zinalenga zaidi katika (a) kukuza ushiriki na mafunzo kwa AZAki; (b) kuweka kumbukumbu na kutoa taarifa za TB, taarifa zilizopatikana na ushuhuda wa mafanikio na (c) kuongeza mawasiliano na teknolojia ili kuwezesha mafunzo yenye tija. Tembelea ukurasa wetu wa Nyaraka zetu ili kujifunza zaidi kuhusu Kifua Kikuu na jitihada zilizofanyika hapa Tanzania na ulimwenguni kote kutokomeza janga la Kifua Kikuu.

Kujenga Uwezo

Utekelezaji wa programu yetu unaenda sambamba na jukumu la kuratibu AZAKi ili ziweze kupambana pamoja na kwa ufanisi juu ya janga la Kifua Kikuu ili kuchangia kufikia malengo na maendeleo ya kitaifa na kimataifa. TTCN inafanya kazi hii kwa (a) kuimarisha na kuongeza kasi ya utekelezaji wa mambo yaliyo ndani ya uwezo wetu ili kupata matokeo zaidi kupitia rasilimali zilizopo (b) kuhamasisha na kushirikisha idadi kubwa ya mashirika na washirika waliopo nchini na kimataifa (c) kuimarisha ubunifu, ushirikiano na muungano kati ya wanachama na washirika katika ngazi mbalimbali. Jiunge Nasi kufahamu watu na mashirika yanayofanya kazi ya kutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu nchini Tanzania.